Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Tikiti za CHAN 2024 zimeanza kuuzwa

CAF kupitia Tovuti yake kwenye ukurasa maalum kwa ajili ya mashindano ya CHAN 2024 imethibitisha kwamba, Tiketi kwa ajili ya kushuhudia michuano ya kandanda ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN)2024 zimeanza kuuzwa kwa umma, zikiwemo katika mataifa mwenyeji Kenya, Tanzania na Uganda. Michuano ya CHAN 2024 itaanza Jumamosi, 02 Agosti 2025.

Michuano ya CHAN 2024 itaandaliwa kwa pamoja na mataifa matatu ya Afrika Mashariki,  Kenya, Tanzania na Uganda, na kuwapa mashabiki katika eneo hili fursa ya kipekee kushuhudia vipaji bora zaidi vya kandanda barani Afrika, Tiketi zinapatikana kwa kununua na ili kupata waweza Kubofya hapa au,

  • Kwa mechi zitakazochezwa TANZANIA – Nunua tiketi zako kwa KUBOFYA HAPA 
  • Kwa mechi zitakazochezwa KENYA - Nunua tiketi zako kwa KUBOFYA HAPA
  • Kwa mechi zitakazochezwa UGANDA - Nunua tiketi zako kwa KUBOFYA HAPA

Bei za tikiti zimepangwa ili kuhakikisha ufikivu na uwezo wa mashabiki kumudu gharama huku zikitoa uzoefu bora kwa wale wanaotafuta huduma za VIP.

Kwa mengi zaidi kuhusu Mashindano ya TotalEnergies CAF African Nations Championship (CHAN) PAMOJA 2024, tembelea www.cafonline.com.