Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Ufuatiliaji na Tathmini

Majukumu ya Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini

  1. Kutathmini na kufuatilia utekelezaji wa Sera, Mpango Mkakati wa Wizara, Mpango Kazi wa Mwaka, Bajeti ya Wizara, Programu na Utekelezaji wa Programu na miradi ya maendeleo inayolenga kutekeleza mipango ya Kitaifa;
  2. Kufuatilia na kutathmini Mipango ya Wizara inayolenga kutekeleza Mipango ya Kitaifa;
  3. Kufuatilia Mipango, Programu na Miradi mbalimbali ya Wizara;
  4. Kutayarisha na kutekeleza mikakati na mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa upande wa Wizara;
  5. Kusimamia utekelezaji wa shughuli za Ufuatiliaji na Tathmini;
  6. Kuandaa taarifa za vipindi maalum zinazohusu Ufuatiliaji na Tathmini kulingana na mipango mbalimbali ya Wizara;
  7. Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Wizara, maelekezo ya Viongozi wa Serikali na Ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM);
  8. Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Wizara yaliyopangwa kwa mujibu wa mpango kazi na yanayojitokeza kwa dharura;
  9. Kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara;
  10. Kuratibu mapitio ya utekelezaji wa shughuli za Taasisi kupitia Mfumo wa PEPMIS; na
  11. Kuratibu na kutunza takwimu mbalimbali za Wizara