Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

UTEUZI WA KAMATI YA TAIFA YA MAANDALIZI YA CHAN 2024 NA AFCON 2027

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Palamagamba Kabudi amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa wadau wa sekta ya habari katika kukuza maendeleo ya taifa, kuimarisha uwazi, na kuhamasisha uwajibikaji.

Mhe. Prof. Kabudi amesema hayo leo Desemba 18, 2024 jijini Dar es Salaam katika mkutano na wadau wa sekta ya habari na utangazaji, ambao amekutana nao kwa lengo la kufahamiana na kushirikiana kutatua changamoto za sekta ya habari.